IQNA

Watetezi wa Palestina

ICC haitekelezi haki kuhusu uhalifu wa kivita

18:53 - December 17, 2023
Habari ID: 3478050
IQNA - Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu yenye makao yake London (IHRC) amekosoa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa undumilakuwili wake linapokuja suala la kushtaki wahusika wa uhalifu wa kivita.

Katika video iliyotumwa kwenye idhaa ya YouTube ya IHRC, Massoud Shadjareh alisema wakati ICC ilitoa hati za kukamatwa Rais Putin wa Russia mara tu baada ya kuzuka kwa vita nchini Ukraine, imefumbia macho jinai za kivita za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi miwili. "Usitarajie ICC kuleta haki ikiwa unatoka nchi zinazoendelea" alisema.

Kwa hakika, aliongeza, ICC haipo kutekeleza haki, lakini ipo kulinda maslahi ya madola ya kikoloni ya Magharibi. Takriban Wapalestina 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya kikatili na ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7.

Hatahivyo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu au Jinai (ICC) yenye makao yake The Hague, Uholanzi haijachukua hatua yoyote dhidi ya watenda jinai wa Israel. Mahakama hiyo inalaumiwa kuwalenga Waafrika  zaidi. Kwa mfano wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007/2008 watu 1,200, Wakenya sita akiwemo rais wa zamani Uhuru Kenyatta na rais wa sasa William Ruto walifikishwa kizimbano kujibu mashtaka. Lakini hivi sasa wakati utawala haramu wa Israel umeua Wapalestina zaidi ya 20,000 wengi wakiwa ni wanawake na Watoto mbali na kuharibu zaidi ya asilimia 60 ya nyumba za Gaza na kubomoa mahospitali, misikiti, makanisa na shule, bado wakuu wa utawala huo, hasa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu hawajachuliwa hatua yoyote.

3486450

Habari zinazohusiana
captcha