IQNA

Kadhia ya Palestina

Vita vya Israel dhidi ya Gaza vyasitishwa kwa muda wa siku 4

19:04 - November 22, 2023
Habari ID: 3477928
TEHRAN (IQNA)- Hatimaye kumefikiwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza kwa muda wa siku nne ili kutoa fursa ya kufikishwa misaada ya kibinadamu na pande mbili kubadilishana mateka.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina "Hamas" imeitangaza katika taarifa yake kwamba, baada ya mazungumzo magumu na tata na marefu, tunatangaza kwamba kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na juhudi kubwa za Qatar na Misri, tumefikia makubaliano ya kibinadamu ya kusitisha mapigano (ya muda mfupi) kwa muda wa siku 4.

Katika muendelezo wa taarifa yake, harakati ya Hamas iimebainisha vipengee vya makubaliano hayo, ambayo kwa mujibu wake, mapigano ya pande zote mbili, shughuli za kijeshi za jeshi la Kizayuni katika maeneo yote ya Gaza, na harakati za magari ya kivita ya utawala huo huko Ghaza zitasimamishwa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mamia ya malori maalumu yaliyobeba misaada ya kibinadamu, misaada ya matibabu na mafuta yataingia katika maeneo yote ya Gaza bila pingamizi.

Aidha taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeeleza kuwa, anawake na watoto 50 wa Israel walio chini ya umri wa miaka 19 wataachiliwa huru mkabala wa wanawake na watoto 150 wa Kipalestina walio chini ya umri wa miaka 19 kwa kuzingatia rekodi za mateka.

Hamas imesisitiza kuwa katika kipindi cha usitishaji vita, utawala unaokalia kwa mabavu umeahidi kutoshambulia au kufanya hujuma dhidi ya mtu yeyote katika maeneo yote ya Ukanda wa Gaza, na watu watakuwa na uhuru wa kuvuka kutoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini kkatika barabara Mtaa wa Salah al-Din.

Katika kipindi cha siku 46 zilizopita, zaidi ya Wapalestina elfu 13 300 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, ambapo elfu 5, 600 ni watoto na elfu 3 500 ni wanawake. Zaidi ya watu elfu 30 wamejeruhiwa hadi sasa. Wanahabari 64 wameuawa shahidi kutokana na vita hivyo. Vituo vya matibabu huko Gaza vimeharibiwa au kufungwa kabisa kwa sababu ya ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo. Vituo vya afya na matibabu vya Gaza pia havifanyi kazi kutokana na kuharibiwa au kukosekana mafuta. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (FAO) limetangaza kuwa karibu watu milioni 2.2 huko Gaza wanahitaji msaada wa haraka wa chakula. Shakhsia na taasisi mbalimbali zimekiri mara kwa mara kwamba, vitendo vya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza ni jinai ya wazi ya mauaji ya kimbari. 

3486120

 

Habari zinazohusiana
captcha