IQNA

Jinai za Israel

Askofu Mkuu wa Canterbury: Israel lazima ikomeshe umwagaji damu huko Gaza

21:12 - November 14, 2023
Habari ID: 3477889
LONDON (IQNA) - Askofu Mkuu wa Canterbury amesema hakuna msingi wowote wa kimaadili unaoweza kuhalalisha mauaji ya Wapalestina huko Gaza ambayo yanatekelezwa na utawala wa Israel.

Vifo vya raia na "janga la kibinadamu" kutokana na mashambulizi ya Israel na kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza haviwezi kuhalalishwa kimaadili, Justin Welby alisema.

"Umwagaji damu lazima ukome", alisema katika Sinodi Kuu ya Kanisa la Uingereza siku ya Jumatatu. Hakuna uhalali wa kimaadili kwa "hasara mbaya ya maisha ya raia" huko Gaza, aliongeza.

Askofu huyo aliongeza kuwa: "... Nataka kuweka wazi kwamba siamini kwamba hasara kubwa ya maisha ya raia na maafa ya kibinadamu yanayotokana na mashambulizi ya Israel na kuzingirwa kwa Gaza yanaweza kuwa ya haki."

Alisema, tangu wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu" kutoka kwake na viongozi wengine wa Kikristo wakati wa ziara ya al-Quds (Jerusalem) zaidi ya wiki tatu zilizopita, "maelfu zaidi ya wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia huko Gaza wameuawa."

"Kwa hiyo narudia wito huo tena kwa uharaka mpya na nguvu zaidi: umwagaji damu huu lazima ukome, mateka lazima waachiliwe na misaada lazima iwafikie wale walio katika Gaza wenye uhitaji mkubwa," Askofu Mkuu alisema.

Tangu Israel ianzishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, idadi ya vifo vya Wapalestina imefikia 11,400, wakiwemo watoto 4,609 na wanawake 3,100. Idadi ya majeruhi ilifikia 28,200, huku 70% wakiwa watoto na wanawake.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, wananchi 3,250 bado hawajapatikana au chini ya vifusi, wakiwemo watoto 1,700.

Aidha hadi sasa katika udondoshaji wake wa mabomu Gaza utawala haramu wa Israel umeharibu kikamilifu misikiti 70, misikiti 153 imeharibuwa  kiasi, na makanisa matatu pia yamelengwa katika mashambulizi ya Israel, likiwemo Kanisa la Porphyrius ambalo ni la tatu kwa ukongwe duniani.

3486015

Habari zinazohusiana
captcha