IQNA

Jinai za Israel

Israel yashambulia Gaza kwa mabomu ya fosforasi, yaendeleza mauaji ya kimbari

16:44 - December 05, 2023
Habari ID: 3477988
TEHRAN (IQNA)- Huku vita vya maangamizi ya kimbari vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza vikiendelea, maafisa wa Palestina wanasema ndege za kivita za utawala huo zimelenga maeneo ya karibu na mji wa Khan Yunis kwa kutumia mabomu ya fosforasi ambayo yanakatzwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Katika siku ya 60 ya vita, utawala haramu wa Israel umepanua operesheni yake ya ardhini kuelekea kusini mwa Ukanda huo.

Pia, ndege za Israel zimeshambulia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, nyingi zikiwa zimejikita mashariki mwa Khan Younis kusini.

Maafisa wa Palestina huko Gaza walisema ndege za Israel zilidondosha mabomu ya fosforasi kaskazini na mashariki mwa Khan Younis.

Kwa mujibu wa habari, familia nzima ziliuawa baada ya kulipuliwa nyumba za Khan Younis na Rafah.

Zaidi ya Wapalestina 15 wameuawa baada ya Israel kushambulia nyumba kadhaa huko Jabalia al-Balad, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na makumi ya wengine kuuawa katika mashambulizi dhidi ya jengo la makazi kusini mwa kitongoji cha Sheikh Radwan huko Gaza.

Wakati huo huo, Dennis Francis, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alirudia wito wake wa mapatano ya kusitishwa mapigano kwa muda mrefu ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuingia Gaza. Katika chapisho kwenye X amesema: "Nimesikitishwa sana na kuhuzunishwa na kuanza tena kwa uhasama Mashariki ya Kati."

Katika habari nyingine kutoka Palestina, jeshi la utawala dhalimu wa Israel limesema askari wake watatu zaidi waliuawa wakati wa mapigano siku ya Jumanne na wengine wanne walijeruhiwa vibaya katika vita mbalimbali kaskazini mwa Gaza.

Zaidi ya wanajeshi 80 wa Israel wameuawa wiki hii huko Gaza tangu kuanza kwa uvamizi wa ardhini katika eneo la Palestina.

Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW) yenye makao yake makuu mjini Washington DC inasema wapiganaji wa Palestina wanaofungamana na Hamas, Jihad Islami, na Kamati za Wananchi wa Palestina wanapambana na vikosi vya Israel huko Gaza kwa kutumia silaha ndogo ndogo, maguruneti ya kurushwa kwa roketi (RPGs),  makombora na mizinga inayolenga vifaru vya Israel.

Takwimu za karibuni zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina zinaonyesha kuwa Wapalestina 15,899, wengi wakiwa ni wanawake na watoto wameuliwa shahidi huku majeruhi wakiongeza hadi elfu 42 tangu kuanza oparesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa Oktoba 7 mwaka huu. 

3486295

Habari zinazohusiana
captcha