IQNA

Waislamu Korea Kusini

Mkorea aliyesilimu kujenga Msikiti huko Incheon

14:46 - April 14, 2024
Habari ID: 3478683
IQNA - Daud Kim, msanii maarufu wa pop wa Korea Kusini na YouTuber ambaye alikubali Uislamu mnamo 2019, ameanza mradi wa kujenga msikiti huko Incheon, Korea Kusini.

Kim, ambaye zamani alijulikana kama Jay Kim, alifichua mipango yake kwenye Instagram, akionyesha kiwanja kilichochukuliwa kwa ajili ya msikiti huo pamoja na mkataba wa ununuzi.

Akielezea matarajio yake, Kim alisema, "Hatimaye nilinunua ardhi kwa ajili ya msikiti huko Korea," na amebainisha maono yake ya siku zijazo ya kuhakikisha "Adhana yenye mvuto itasikika katika kila barabara nchini Korea."

Anakusudia kuanzisha sio tu mahali pa kuabudia bali pia studio ya podikasti ya Kiislamu inayotolewa kwa ajili ya Da'wah, akilenga kufikia Wakorea.

Akitambua changamoto zilizopo, Kim bado ana matumaini kuhusu mpango huo lakini akataja haja ya msaada wa kifedha ili kufanikisha ujenzi wa msikiti huo. Amefungua jukwaa la michango ili kusaidia katika kukamilisha mradi huo.

Huko Korea Kusini, Waislamu ni sehemu ndogo ya idadi ya watu, wengi wao wakiwa ni wahamiaji, wafanyakazi na wanafunzi wa kimataifa. Msikiti wa kwanza nchini humo, Msikiti wa Kati wa Seoul, ulianzishwa mwaka 1976, na tangu wakati huo, idadi ya misikiti imeongezeka na kujumuisha misikiti 15 iliyosajiliwa rasmi na takriban maeneo 150 hadi 200, yanayotumika kama kumbi ndogo za ibada. Mchango wa Kim unaashiria nyongeza muhimu kwa miundombinu ya Kiislamu katika taifa hilo.

Kim, ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la Jay Kim, alisilimu mnamo Septemba 2019 na akatangaza kusilimu kwake kwenye video ya YouTube.

3487929

captcha