IQNA

Kadhia ya Palestina

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Mrengo wa mapambano ya Kiislamu umabadilisha dunia

18:01 - November 03, 2023
Habari ID: 3477832
TEHRAN (IQNA)- Akizungumza leo katika sala ya Ijumaa ya mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimeen Kazem Sediqi amesema kuwa leo mrengo wa mapambano ya Kiislamu ni mrengo wa kimataifa na kuongeza kwamba mrengo huo umabadilisha dunia.

Akizungumza katika hotuba za sala hiyo iliyosimamishwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimeen Kazem Sediqi amesema kwamba matukio yanayoshuhudiwa katika mrengo wa mapambano hayo yanatokana na mafundisho ya chuo cha Wilaya na Uimamu, ambayo bendera yake leo iko mikononi mwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Khatibu huyo wa swala ya Ijumaa ya mjini Tehran ameashiria kupasishwa sheria ya kuruhusu vita dhidi ya utawala ghasibu wa Israel katika bunge la Algeria na kusema kila siku pande mpya zinaendelea kujiunga na mrengo wa mapambano kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kupambana na utawala huo wa kibaguzi. Ameelezea matarajio yake kwamba serikali za Kiislamu, kama alivyosema Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, zitakata uhusiano wao na kuwafukuza mabalozi wote wa utawala huo bandia na hatimaye kuuwekea vikwazo vya pande zote.

Hujjatul Islam Sediqi, huku akisisitiza kuwa kadhia muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu leo ni suala la Ghaza, amesema kwamba Umma wa Kiislamu unapasa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu, uwauge mkono mujahidina waliojitolea katika uwanja wa mapambano na kuwasaidia kwa hali na mali watu wanaodhulumiwa wa Ghaza kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Utawala wa Israel umekuwa ukiendesha vita vya kinyama dhidi ya Ghaza tangu tarehe 7 Oktoba, wakati makundi ya muqawama wa Palestina yakiongozwa na Hamas yalipoanzisha operesheni yao kubwa zaidi dhidi ya utawala wa Kizayuni katika kipindi cha miaka mingi iliyopita. Shambulio hilo la kishujaa lililopewa jina la operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa, lilitekelezwa kujibu jinai za utawala huo zilizokithiri dhidi ya watu wa Palestina.

Vita vya utawala ghasibu wa Israel hadi sasa vimepelekea kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina 9,000 wasio na hatia na kuwaacha wengine zaidi ya 32,000 wakijeruhiwa.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa wingi wa kura azimio linalotoka kutekelezwa mara moja "usitishaji vita wa kibinadamu" huko Gaza. Utawala wa Israel umekataa miito yote ya kusitisha mapigano kwa madai kuwa itawanufaisha wapiganaji wa Hamas.

4179565

Habari zinazohusiana
captcha