IQNA

Watetezi wa Palestina

Leo dunia imetambua usahihi wa msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Palestina

20:21 - December 08, 2023
Habari ID: 3478008
TEHRAN (IQNA)-Imamu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameashiria mpango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kutatua kadhia ya Palestina kwa njia ya kura ya maoni kwa msingi wa "kila Mpalestina ana kura moja", na kusema: Maneno yetu ni ya kimantiki na ya kidemokrasia.

Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khatami ameyasema hayo katika hotuba ya Sala ya Ijumaa ameendela kusema kwamba yanayojiri katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, stratijia ya Iran tangu mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu ni kwamba Israel inapaswa kuondoka katika eneo la Magharibi mwa Asia, Palestina ni mali ya Wapalestina na kwamba kura ya maoni inapaswa kufanyika ili kuamua hatma ya Palestina. Aidha Hujjatul Islam Khatami amesema: Miaka 75 imepita tangu jinai Israel ianzishe jinai Palestina na leo dunia imetambua usahihi wa msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Amesisitiza kuwa: Leo hii, hata katika nchi ya Uingereza, ambayo ilikuwa na nafasi katika kuanzishwa utawala bandia wa Israel, maelfu ya watu wanatoa nara ya "mauti kwa Israeli".

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema: "Wakati mmoja, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alikuwa akizungumzia suala la kubuniwa "Mashariki ya Kati Mpya", lakini leo hii, Mashariki ya Kati Mpya imeundwa kwa msingi wa muqawama ambao umevurunga mlingano wa nguvu katika eneo hilo."

4186603

captcha