IQNA

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran

Ukoo wa Aal Saud haustahiki kusimamia Haram Mbili Tukufu

1:17 - May 28, 2016
Habari ID: 3470341
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa utawala wa Aal Saud haustahiki kusimamia Haram Mbili Tukufu za Makka na Madina.

Atayatullah Sayyid Ahmad Khatami aidha ameukosoa utawala wa Aal Saud ambao unakwamisha juhudi za Waislamu wa Iran za kwenda Hija mwaka huu na kuongeza kuwa, haram mbili hizo tukufu zinapaswa kusimamiwa na timu ya wataalamu kutoka serikali za Kiislamu.

Ayatullah Khatami ameashiria namna utawala wa Aal Saud unavyofanya ukaidi usio na maana mbele ya haki ya wananchi wa Iran wanaofanya juhudi za kuhakikisha wanashiriki katika ibada ya Hija mwaka huu na kueleza kuwa, wasimamiaji wa haram hizo tukufu hawapasi kufanya kazi kwa malengo ya madola ya kibeberu na Wazayuni.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya jiji la Tehran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka kuona mahujaji wakidhaminiwa usalama wao na kutovunjiwa heshima na kwamba mahujaji wa Iran hawawezi kushiriki ibada ya Hija wakiwa katika hali ngumu na ukosefu wa usalama.

Ayatullah Khatami pia ameashiria njama za Marekani za kujipenyeza ndani ya Iran kupitia kuishinikiza Tehran ikubali kuwa na uhusiano na Marekani, kujipenyeza katika vyombo vya uchukuaji maamuzi, kuwagawa wananchi katika matabaka mawli na kuharibu nyenzo za nguvu katika mfumo wa Kiislamu na kubainisha kuwa, njia pekee ya kukabiliana na njama hizo ni kuendesha muqawama na kusimama kidete mbele ya uistikbari. Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa, katika kipindi cha siku si nyingi zijazo, tutashuhudia demokrasia ya kiliberali ya Magharibi ikigonga mwamba sawa kabisa na ulivyosambaratika Uliberali wa kijamii wa Mashariki, na kuzidi kunawiri Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.


captcha