IQNA

Kuhifadhi Qur'ani Tukufu

Wahifadhi 143 wa Qur’ani Tukufu waenziwa Ukanda wa Gaza

21:16 - October 31, 2022
Habari ID: 3476011
TEHRAN (IQNA) – Katika sherehe katika ardhi ya Palestina ya Ukanda wa Gaza, wahifadhi 143 wa Qur’ani Tukufu wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya watu na maafisa wa serikali.

Sherehe hiyo ilifanyika Alhamisi usiku katika mikoa ya kaskazini ya ukanda huo ambao uko chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala haramu wa Israel.

Sherehe hiyo  iliandaliwa kwa wakati mmoja na kuwakumbuka mashahidi 44 wa eneo hilo, wote kutoka kwa familia ya Al-Batsh, ambao waliuawa wakati wa uvamizi wa utawaladhalimu  Israeli wa 2014 huko Gaza.

Wahifadhi wote wa Qur’ani pia walitoka katika familia hii na walipokea tuzo katika hafla hiyo.

Mmoja wao aitwaye Afnan Al-Batsh alishinda safari ya Umrah.

Wakuu wa vituo vya Qur'ani vya Ghaza pamoja na wawakilishi wa makundi ya Wapalestina walishiriki katika hafla hiyo.

Shughuli za Qur’ani ni za kawaida sana katika Ukanda wa Gaza na programu za usomaji na kuhifadhi  Qur’ani hufanyika katika eneo hilo mwaka mzima.

Huko nyuma mwanzoni mwa Septemba, jumuiya ya Dar-ol-Quran na Sunnah katika Ukanda wa Gaza iliandaa hafla ya kuwaenzi wahifadhi 580 wa Qur'ani.

 

Tangu mwaka 2006 utawala wa Kizayuni wa Israel umeliweka eneo la Ukanda wa Gaza chini ya mzingiro wa pande zote. Sababu kuu ya mzingiro wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza ni ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika uchaguzi wa Bunge la Palestina. 

Kutokana na mzingiro huo, Gaza imekumbwa na maafa makubwa. Kuzingirwa kwa miaka 15 eneo la Gaza kumesababisha uhaba wa chakula katika eneo hilo kiasi kwamba, Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la umoja huo (FAO) pia wameeleza wasiwasi wao kuhusu suala hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kisiasa na Kiuchumi cha Palestina, mwaka 2021 zaidi ya nusu ya familia za Wapalestina hazikuwa na usalama wa chakula.

4095085

captcha