IQNA

Waungaji mkono Palestina

Maandamano makubwa zaidi Cape Town kuunga mkono Palestina na kulaani Israel

10:37 - November 12, 2023
Habari ID: 3477879
CAPE TOWN (IQNA) – Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ulishuhudia maandamano makubwa zaidi katika jiji hilo katika miaka kadhaa wakati makumi ya maelfu ya watu walikusanyika kutangaza mshikamano na Palestina, wakitaka kukomeshwa kwa ukatili wa Israel huko Gaza.

Umati mkubwa wa watu uliandamana katikati mwa jiji la Cape Town siku ya Jumamosi, wakitoa wito wa kusitishwa kwa vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Ilikuwa ni moja ya maandamano makubwa katika jiji hilo kwa miaka kadhaa, na yamkini yalizidiwa ukubwa na maandamano mengine yaliyowahi kufanyika  kupinga vita vya awali vya Israel dhidi ya Gaza.

Maandamano hayo yalianza katika Msikiti wa Muir Street katika Wilaya ya Sita na kuishia katika bunge la mkoa wa Western Cape katika mtaa wa Wale.

Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na mashirika kadhaa ya kiraia na vyama vya kisiasa, yanakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya utawala dhalimu wa Israel kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya watu katika Ukanda wa Gaza, ambapo hadi sasa Wapalestina zaidi 11,000 wameuawa aghalabu wakiwa ni  watoto na wanawake. Utawala wa Israel pia inatekeleza mzingiro wa kinyama wa pande zote dhidi ya Gaza.

Walowezi wa Kizayuni na wanajeshi wa Israel pia wamekuwa wakiwashambulia Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi, na karibu Wapalestina 200 wameuawa huko tangu Oktoba 7.

Waandamanaji walijipanga katika mitaa ya Cape Town wakiwa na bendera na mabango yaliyoandikwa: "Kwa milioni, kwa bilioni, sisi sote ni Wapalestina" na "Kutoka mto hadi Baharini, Palestina itakuwa huru."

Pia kulikuwa na nara zilizoelekezwa kwa Rais wa Marekani Joe Biden, kama vile "Je, umeua watoto wangapi leo?"

Mwanzoni mwa maandamano hayo, waandaaji walitoa wito wa nidhamu na kuwakumbusha hadhirina kwamba hawakuwa wapinga Wayahudi, bali ni Wazayuni. Waandamanaji pia walitoa nara za kuunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Taarifa kutoka Muungano wa Afrika Kusini wa Kususia Utawala wa Kizayuni wa Israel (BDS) siku ya Ijumaa ilisema kwamba watu huko Gaza walikuwa wakifa njaa. Walitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuwasilishwa kwa wingi misaada ya kibinadamu huko Gaza.

Padre Michael Weeder, Mkuu wa Kanisa Kuu la St George, alihutubia waandamanaji. Alitoa wito kwa viongozi wa dunia kuacha kutumia fedha katika vita na badala yake waelekeze fedha zaidi katika kuleta amani. Mchungaji Allan Boesak, mwanaharakati mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi, alitoa wito kwa serikali ya Afrika Kusini kumtimua balozi wa utawala haramu wa Israel nchini humo.

Kumekuwa na matukio kadhaa ya mshikamano na Wapalestina mwishoni mwa juma. Siku ya Ijumaa usiku, ibada ya Shabbat iliandaliwa na Wayahudi wa Afrika Kusini kwa ajili ya Palestina Huru kwenye ufuo wa Sea Point. Lilikuwa tukio la nne kama hilo, na waandaaji wanasema wanapanga kulipeleka katika maeneo mengine ya jiji katika wiki zijazo.

Siku ya Jumamosi asubuhi, kundi la wanaharakati pia waliweka mabango kwenye ufukwe wa Sea Point ya watoto wa Kipalestina ambao walikuwa wameuawa katika mzozo hadi sasa.

3485970

Habari zinazohusiana
captcha