IQNA

Umoja wa Mataifa wafumbia macho ukatili wa Israel dhidi ya watoto

12:24 - June 10, 2015
Habari ID: 3312923
Katika hatua ya kushangaza, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekataa kuuoredhesha utawala haramu wa Israel na ambao unaendelea kuua watoto wa Ukanda wa Gaza, katika orodha ya tawala zinazovunja haki za watoto duniani.

Ban Ki-moon amechukua msimamo huo katika hali ambayo ripoti nyingi za siri ambazo zimekuwa zikiwasilishwa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu likiwemo la Human Rights Watch, zimeuweka wazi utawala huo haramu katika orodha ya tawala zinazokiuka haki za watoto, kutokana na jinai zake za wazi dhidi ya watoto wa Palestina. Kuhusiana na suala hilo Leila Zerrougui, Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watoto katika Maeneo ya Vita, kwa mara ya kwanza ametaka kuwekwa jeshi la utawala wa Israel katika orodha nyeusi ya umoja huo. Kila mwaka majina ya nchi zinazokiuka haki za watoto wakati wa vita huwekwa kwenye orodha hiyo. Katika orodha nyingi zinazotolewa na taasisi tofauti za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu, utawala ghasibu wa Israel umetajwa kuwa katika mstari wa mbele wa serikali zinazotekeleza jinai na kukiuka wazi haki za watoto katika maeneo ya vita. Kuhusu suala hilo Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema kuwa katika vita vyake vya kichokozi vya siku 50 huko katika Ukanda wa Gaza mwaka uliopita, utawala katili wa Israel uliua kinyama watoto 539 wa Kipalestina na kujeruhi wengine 2956. Mbali na unyama huo utawala wa Israel bado unawashikilia mamia ya watoto wa Kipalestina katika jela zake za kuogofya na kukiuka wazi haki zao za kimsingi katika jela hizo. Vitendo hivyo ni mfano wa wazi wa ukiukaji wa haki za binadamu na mauaji ya kizazi na kukiri taasisi tofauti za Umoja wa Mataifa kuhusu jambo hilo ni uthibitisho wa wazi wa ukweli huo mchungu. Kwa msingi huo, jamii ya kimataifa inataka kuona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi ya utawala huo katili bila ya kufanyiwa upendeleo wa aina yoyote. Kuzembea Umoja wa Mataifa katika kutekeleza majukumu yake kuhusiana na utawala wa Israel umeufanya utawala huo umee pembe na hivyo kuendelea kuvunja haki za kimsingi kabisa za taifa la Palestina na mataifa mengine katika Mashariki ya Kati. Licha ya matakwa ya jamii ya kimataifa ya kutaka utawala wa kibaguzi wa Israel ufikishwe mbele ya vyombo vya sheria kutokana na jinai zake dhidi ya watu wasio na hatia wa Palestina na hasa ukiukaji wa haki za watoto katika Ukanda wa Gaza, lakini hakuna hatua zozote za kisheria ambazo zimewahi kuchukuliwa dhidi ya utawala huo kutokana na uungaji mkono na upendeleo wa wazi unaoonyeshwa na nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu, kwa utawala huo.../

3312760

Habari zinazohusiana
captcha