IQNA

Uchumi Halal

Istanbul yaanandaa Mkutano wa ‘Halal’ na Maonyesho ya OIC ya ‘Halal’

20:06 - November 24, 2023
Habari ID: 3477940
ISTANBUL (IQNA) - Mamia ya makampuni na mashirika yanayoongoza kutoka nchi 40 yanashiriki katika Mkutano wa Halal wa Dunia na Maonyesho ya Halal ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), ambayo yalifunguliwa Alhamisi huko Istanbul, ili kuonyesha bidhaa na huduma zao katika soko la halal la kimataifa, lenye thamani ya zaidi ya dola trilioni 7.

Mkutano wa Halal Ulimwenguni, ambao unafanyika wakati huo huo na maonyesho, unalenga kushughulikia maswala na uwezekano wa uchumi halal, kama vile athari za maadili na kijamii, mwelekeo wa sasa na wa siku zijazo, faida na hatari, na uwezo wa ubunifu na kisanii. Mada ya mkutano wa kilele wa mwaka huu ni 'Lango la Uchumi wa Halal Ulimwenguni: Tambua na Ufungue Uwezo.’

Yunus Ete, mkuu wa Baraza la Mkutano wa Halal Ulimwenguni, alisema kuwa maonyesho hayo ni moja ya majukwaa muhimu ya ushirikiano wa kibiashara. Pia alisema kuwa soko la Halal linatarajiwa kufikia dola trilioni 10 katika miaka mitano ijayo, na kwamba kuna mahitaji makubwa ya watumiaji wa bidhaa za chakula zenye afya, halali na za asili.

Mkutano wa Halal wa Dunia na Maonyesho ya Halal ya OIC ni mikusanyiko miwili mikuu ya bidhaa na huduma ambazo zinatayarishwa na kuwasilishwa kwa mujibu wa  miongozo ya Kiislamu (yaani halal), ambayo hufanyika kila mwaka huko Istanbul tangu 2014.

Kulingana na Ripoti ya Uchumi wa Halal ya OIC, Uturuki, Indonesia na Malaysia zimeweza kuwa miongoni mwa wauzaji 20 wakuu wa bidhaa za halal duniani.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ni jumuiya ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1969, yenye nchi wanachama 57, huku 48 zikiwa ni nchi zenye Waislamu wengi."

3486146

Kishikizo: uchumi halal mkutano
captcha