IQNA

Mkutano wa kimatiafa wa "Mahdaviyyat" wafanyika Tehran

10:08 - June 01, 2015
Habari ID: 3309948
Kongamano la 11 la Kimataifa la Itikadi ya Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) limeanza Jumapili hii hapa mjini Tehran na kushirikisha pamoja shakhsia mbalimbali wa ndani na nje ya Iran

Shakhsia mbalimbali wameshiriki kwenye ufunguzi huo, viongozi wa ngazi mbalimbali wa Iran pamoja na wanafikra na wasomi kutoka nchi 52 duniani.
Sheikh Muhammad Hassan Abu Turabifar, Naibu Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amezungumza kwenye sherehe hizo za ufunguzi na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwaunga mkono wanyonge na watu wanaodhulumiwa ikiwa ni pamoja na wananchi wa Yemen, Palestina na Iraq.
Amesema msimamo huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Kongamano hilo linatarajiwa kumalizika leo Jumatatu.../mh

3309537

Kishikizo: mahdi imam mkutano tehran
captcha