IQNA

Jinai za Israel

ISESCO yalaani mashambulizi ya Israel kwenye Shule za Gaza na kuyataja kuwa 'Aibu kwa Ubinadamu'

17:10 - November 20, 2023
Habari ID: 3477917
RABAT (IQNA) - Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (ISESCO) limetoa tamko kali siku ya likilaani mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya shule mbili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuwa ni "fedheha kwa ubinadamu" na "uhalifu wa kutisha".

ISESCO ambayo ni taasisi tanzu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilieleza mshikamano wake na wananchi wa Palestina na kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kukiuka sheria na kanuni za kimataifa kwa kulenga vituo vya kiraia.

Jeshi la Israel lilishambulia kwa mabomu Shule ya Al-Fakhoura na Shule ya Tal Al-Zaatar siku ya Jumamosi, na kuua na kuwajeruhi zaidi ya Wapalestina 200 waliokuwa wamejihifadhi humo kutokana na uvamizi unaoendelea wa Israel huko Gaza.

Shule ya Al-Fakhoura inaendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutoa Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) na iko katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia. Shule ya Tal Al-Zaatar iko katika mji wa Beit Lahia.

ISESCO ilisema kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya shule hizo ni "vitendo vya kinyama" ambavyo vilionyesha utawala katili wa Israel "unapuuza mitazamo ya watu kote ulimwenguni"  ambao wanapinga ukatili wake huko Gaza. Shirika hilo pia lilisema kuwa utawala dhalimu  wa Israel ulikuwa ukitumia zana zake za kivita kushambulia watoto na limeitaka jumuiya ya kimataifa hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti za kukomesha ukatili wa Israel na kuwalinda raia wa Palestina na haki zao.

Kitendo cha Israel cha kushambulia kwa mabomu shule za Al-Fakhoura na Tal Al-Zaatar kimezusha hasira na shutuma kutoka kwa mataifa na jumuiya mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na makundi ya haki za binadamu na wanaharakati.

Vita vya maangamizi ya umati vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza vilianza tangu Oktoba 7 na hadi sasa vimesababisha vifo vya Wapalestina 13,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mashambulizi hayo yalianza baada ya kundi la kupigania ukombozi wa  Palestina la Hamas kuanzisha operesheni ya kushtukiza katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ilkiwa ni jibu kwa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na vitendo vya utawala huo ghasibu vya kuuvunjia heshima  Msikiti wa al-Aqsa.

3486092

Habari zinazohusiana
captcha