IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Maonyesho ya Qur’ani ya mwezi Ramadhani yanaendelea nchini Thailand

15:57 - March 23, 2024
Habari ID: 3478559
IQNA - Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Thailand kimefanya maonyesho ya Qur'ani katika Kituo cha Kiislamu cha Bangkok.

Maonyesho hayo yameandaliwa kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Warsha kuhusu kaligrafia ya Qur'ani pia inaendelea katika maonyesho hayo kwa kushirikisha mtaalamu wa kaligrafia wa Iran.

Kituo cha Utamaduni cha Iran pia kimemwalika qari kutoka Iran kusoma Quran katika misikiti ya Shia na Sunni ya Thailand.

Pia inapanga hafla maalum katika nyusiku za Laylatul Qadr (siku za 19, 21 na 23 za Ramadhani).

Hujjatul Islam Seyed Abdol Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija na Ziyara atakuwepo katika sherehe hizo.

Kongamano kwa mnasaba wa siku ya kimataifa ya Quds ni miongoni mwa programu nyingine za kituo cha Ramadhani.

Pia imechapisha jarida maalum la kidijitali kuhusu Ramadhani na vile vile kitabu cha kielektroniki cha kuhusu Saumu ya Ramadhani.

4206699

Kishikizo: ramadhani Thailand
captcha