IQNA

Qur'ani Tukufu

Iran yafungua maonyesho ya Qur'ani Tukufu huko Bangkok

21:26 - February 07, 2024
Habari ID: 3478317
IQNA - Maonyesho yanayoangazia kazi za sanaa za Qur'ani Tukufu na bidhaa husika kutoka Iran yamezinduliwa katika mji mkuu wa Thailand wa Bangkok.

Maonyesho hayo ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa kadhaa wa Iran na Thailand akiwemo Balozi wa Iran nchini Thailand Seyyed Reza Nobakhti, mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Thailand Mehdi Zare, na Naibu wa Waziri  wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani Tukufu Alireza Moaf.

Mwanzoni mwa hafla hiyo, Mohammad Mehdi Azizzadeh, afisa wa Wizara ya Utamaduni ya Iran alitoa maelezo mafupi ya kazi za sanaa, bidhaa za Qur'ani na vitabu  katika maonyesho hayo.

Akihutubia pia hafla hiyo, Phonpoom Vipattipumiprates, Naibu Waziri wa Utamaduni wa Thailand, alisifu utamaduni "tajiri" wa Iran, akibainisha kuwa nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano mkubwa wa kiutamaduni tangu kuanza kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1955.

Hafla hiyo inayoangazia sanaa ya kisasa ya Qur'ani ya Iran, itasaidia kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiutamaduni na Kiislamu kati ya mataifa hayo mawili, alisema.

Moaf pia alihutubia tukio hilo, akibainisha kuwa maonyesho hayo yanaweza kupanuliwa kwa njia nyinginezo ikiwa Thailand iko tayari.

Maonyesho hayo yatakamilika Februari 11, 2024.

 

4198356

captcha