IQNA

Watetezi wa Palestina

Al-Azhar yanaonya kuhusu maafa ya kibinadamu katika mji wa Rafah huko Gaza

17:31 - February 14, 2024
Habari ID: 3478350
IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza, na kuonya kuhusu maafa ya binadamu katika eneo hilo.

Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar kimesema katika taarifa yake kwamba, mipango hatari ya utawala ghasibu wa Israel wa kufanya uvamizi wa nchi kavu mjini Rafah, ambapo Wapalestina wapatao milioni 1.5 waliokimbia makazi yao wametafuta hifadhi, itasababisha maafa makubwa ya kibinadamu.

Ikirejelea miito ya kimataifa ya kulaani jinai za Wazayuni, taarifa hiyo ilikariri haja ya mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kuungana dhidi ya uvamizi wa Rafah.

Kushindwa kuwasaidia Wapalestina haraka kunaweza kusababisha kuuawa shahidi maelfu ya watu wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, ambao wamejificha Rafah wakihofia mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Israel.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu katili wa utawala wa Israel hivi karibuni alisema uvamizi wa ardhini dhidi ya Rafah utaanzishwa ndani ya wiki mbili.

Wakati utawala huo umeshindwa kufikia malengo yake yoyote katika vita vya Gaza, katili Netanyahu alilitaka jeshi kuangamiza harakati ya Hamas huko Rafah kabla ya kuanza kwa mwezi wa Ramadhani.

Wakati huo huo, televisheni ya Israel Channel 12 imefichua tofauti inayojitokeza kati ya Netanyahu na mkuu wa jeshi la Israel kuhusiana na uvamizi wa Rafah.

Imeripotiwa pia kuwa Marekani imeitaka Israel kuepuka kuishambulia Rafah hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hamas, Iran, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Qatar pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya pia zimeonya dhidi ya uvamizi wa Rafah.

Mashambulio makali ya utawala wa Israel katika maeneo ya Rafah yenye msongamano wa watu Jumapili usiku yaliwaua zaidi ya Wapalestina 100.

Mashambulizi ya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza uliozingirwa tangu mwezi Oktoba yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 28,500 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwaacha wengine zaidi ya 68,000 wakijeruhiwa.

3487190

Habari zinazohusiana
captcha