IQNA

Kadhia ya Palestina.

Ayatullah Khamenei: Wapalestina Gaza wanapambana na uistikbari, Marekani

19:05 - January 03, 2024
Habari ID: 3478140
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema mpaka wa ulimwengu wa Kiislamu uko Gaza hivi leo, na kwamba Wapalestina wa eneo hilo wamesimama dhidi ya kiburi au mfumo wa kiistikbari na Marekani.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumatano wakati alipoonana na maelfu ya wasomaji kasida na mashairi ya Ahlul Bayt AS. Sambamba na kutoa mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Bibi Fatimatuz Zahra SA amesisitiza kuwa, kuadhimisha siku ya kuzaliwa Imam Khomeini (MA) ambaye ni mbeba bendera ya Jihadi ya Bibi Fatima SA kunakumbushia jitihada na jihadi kubwa za Luteni Jenerali Qassem Soleimani (aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC).

"Mpaka wa ulimwengu wa Kiislamu leo uko Gaza, hisia za ulimwengu wa Kiislamu zko Gaza leo, na Wapalestina huko wamesimama dhidi ya ulimwengu wa ukafiri, dhulma,uistikbri na dhidi ya Marekani," Kiongozi Muadhamu amesema

Utawala katili wa  Israel umekuwa ukiendesha vita vikali katika Ukanda wa Gaza tangu mwezi Oktoba na kuua watu wasiopungua 22,313 wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Zaidi ya wengine 57,000 pia wamejeruhiwa.

Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, rais wa Marekani ametangaza waziwazi kwamba yeye ni Mzayuni akiwa ni maana kwamba ule ukhabithi wote mchafu walio nao Wazayuni, na yeye pia anao.

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Bibi Fatimatuz Zahra aliweka jiwe la msingi la Jihadi ya kubainisha ukweli na kusisitiza kuwa, wasomaji wa kasida na mashairi ya Ahlul Bayt AS wanapaswa kuendelea kuifanya kigezo chao bora jihadi hiyo na somo kubwa linalopatikana ndani yake. 

Aidha amesema, mkakati mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha miaka 45 iliyopita ni kutegemea nguvu laini na nguvu hizo zinapaswa zifanywe kubwa zaidi.

Ameongeza kuwa, Jihadi ya kubainisha ukweli na uhalisi wa mambo mbali na nguvu zake za kutikisa nyoyo na kuleta harakati za kimapinduzi, iko makini pia katika kuainisha malengo muhimu zaidi kwani baadhi ya wakati katika sehemu ambayo panahitajika mno umoja na mshikamano katika Ulimwengu wa Kiislamu kunafanyika uzembe na kuishia kwenye kuzuka mizozo na migogoro katika safu za Waislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, vile vile amesema, miongoni mwa athari za nguvu hizo laini za Iran ni kukimbia kwa madhila Marekani huko Afghanistan na kuchukiwa mno dola hilo la kibeberu na wananchi wa Iraq. 

3486674

Habari zinazohusiana
captcha