IQNA

Mwezi wa Ramadhani na utamaduni

Utamaduni wa jadi katika Haram ya Imam Ridha (AS) Kuashiria kuwadia Ramadhani

22:34 - March 12, 2024
Habari ID: 3478496
IQNA - 'Hal Hilalik Ya Ramadan', ni tukio la jadi ambalo limezoeleka katika nchi nyingi za Kiarabu kwa ajili ya kukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Tukio hilo la kiutamaduni limeandaliwa katika haram ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran Jumatatu usiku.

Hujjatul Islam Seyed Mohammad Zolfaqari, mkurugenzi wa idara ya wafanya ziara wasio Wairani ya Astan Quds Razavi (Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha AS) , aliiambia IQNA kwamba watoto 40 na vijana kutoka nchi 12 wamehudhuria sherehe hiyo.

Hafla hiyo imefanyika katika Rawaq zote (nafasi zenye paa zilizounganishwa na Haram tukufu), alibainisha.

Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, hafla hiyo inawashirikisha watoto na vijana wakiimba qasida za  kuwasifu Ahl-ul-Bayt (AS), na kuwapongeza Waislamu kwa kuwasili kwa Ramadhani na kuwakumbusha watu baraka za mwezi huu mtukufu.

Amesema ibada hiyo inafanyika katika madhabahu tukufu ya Imam Reza (AS) kwa mwaka wa pili mfululizo kwa lengo la kuziweka hai mila hizo njema na kuchangia katika kusambaza thamani za Kiislamu kwa vizazi vijavyo.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ulianza Jumatatu katika baadhi ya maeneo ya dunia na Jumanne katika maeneo mengine kwa kutegemea mwezi mwandamo.

3487520

captcha