IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Matukio yaliyopangwa kwa washindani pembeni ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

20:40 - February 18, 2024
Habari ID: 3478373
IQNA - Programu kadhaa zimepangwa kando ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.

Programu hiyo imeandaliwa kwa  wagombea na wajumbe wa jopo la majaji.

Tehran ni mwenyeji wa Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran kwa kushirikisha wahifadhi na wasomaji 99 kutoka nchi 44.

Sambamba na hayo, Awamu ya 8 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi wa Shule inaendelea katika mji mkuu wa Iran.

Washiriki wa hafla zote mbili za Qur'ani Tukufu na wajumbe wa jopo la majaji au waamuzi walifanya ziara katika kaburi la Imam Khomeini (RA), marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huko  Rey,kusini mwa Tehran, siku ya Ijumaa.

Kama mpango mwingine wa kando, wametembelea Bustani ya Makumbusho Kujihami Kukatifu siku ya Jumamosi na  Husseiniyah Jamaran , nyumba ya hayati Imam Khomeini (RA) kaskazini mwa Tehran siku ya Jumapili.

Siku ya Jumatatu, wamepangwa kutembelea Mnara wa Milad, mnara mrefu zaidi nchini Iran.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hafla ya kila mwaka ambayo huwavutia wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

4200097

 

Habari zinazohusiana
captcha