IQNA

Msomaji Qur'ani

Qari Mahmoud Shahat Anwar wa Misri amsifu baba mzazi kama mfano wake wa kwanza wa kuigwa

20:10 - January 13, 2024
Habari ID: 3478192
IQNA - Mahmoud Shahat Anwar, qari maarufu wa Misri ambaye ni mtoto wa marehemu msomaji wa Qur'ani Sheikh Shahat Muhammad Anwar, alimuelezea baba yake kama mfano wake wa kwanza wa kuigwa na chanzo cha mwongozo.

"Alinifundisha jinsi ya kubaki imara mbele ya mawimbi ya maisha yanayovuma," alisema katika mahojiano juu ya kumbukumbu ya miaka 15 ya kifo cha Sheikh Shahat Muhammad Anwar.

Mahmoud aliongeza kuwa malezi yake ya Qur'ani Tukufu na mapenzi na heshima yake kwa Kitabu Kitukufu yalipatikana kutokana na juhudi za baba yake.

Shahat Muhammad Anwar alikuwa mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri ambaye alipata umaarufu katika umri mdogo kwa sababu ya kipaji chake katika fani hii.

Shahat alizaliwa Julai 1950 katika kijiji cha Kafr el-Wazir katika Jimbo la Dakahlia nchini Misri. Alimpoteza baba yake alipokuwa na umri wa miezi mitatu.

Anwar alianza kujifunza Qur'ani Tukufu akiwa na umri mdogo na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Alipokuwa na umri wa miaka kumi, ami yake alimpeleka katika kijiji cha Kafr el-Maqam ili kujifunza usomaji wa Tajweed pamoja na Mwalimu Seyed Ahmed Fararahi.

Alijifunza usomaji wa Qur'ani Tukufu na punde akawa qari maarufu.

Maustadh Qur'ani kama Said Abdul Samad al-Zanani na Hamdi Zamil walikuwa miongoni mwa wale walioanza njia ya usomaji wa Qur'ani baada ya kuhudhuria duru za usomaji Qur'ani za Sheikh Shahat.

"Kwa kuhifadhi Qur'ani (katika utoto), nilihisi nimefikia furaha isiyoelezeka," alisema. "Baada ya hapo, kwa sababu nilikuwa na sauti nzuri na Lahn yangu ilikuwa kama ile ya maustadh wakuu, ... nilijulikana kama "ustadh mdogo".

Egyptian Qari Mahmoud Shahat Anwar Praises Father as His First Role Model

Kisha akaalikwa kusoma Qur'ani Tukufu katika kipindi ambacho kilihudhuriwa pia na Kamil al-Balouhi, mkuu wa Redio ya Qur'ani ya Misri wakati huo.

Al-Balouhi alimwalika asome Kurani kwenye Redio na aliingia kwenye Redio ya Kurani mnamo 1979.

Shahat Muhammad Anwar alisafiri katika nchi nyingi kama Hispania, Ufaransa, Marekani, Nigeria, Cameroon, Argentina, na Uingereza, kwa ajili ya usomaji wa Qur'ani.

Wanawe watatu na binti sita wote ni wahifadhi wa Quran. Wanawe Anwar na Mahmoud pia ni maqari mashuhuri.

Kwa sababu ya ugonjwa wa ini, hakuweza kusoma Qur'ani hadharani katika miaka minne ya mwisho ya maisha yake.

Sheikh Shahat alifariki Januari 13, 2008 akiwa na umri wa miaka 58 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Ifuatayo ni qiraa yake ya Aya za 38-40 ya Surah At-Tawbah ya Qur'ani Tukufu:

 

 

3486789

captcha