IQNA

Qiraa yenye mvuto ya Qur'ani Tukufu ya Shahat Muhammad Anwar

17:28 - September 19, 2020
Habari ID: 3473184
TEHRAN (IQNA) – Hivi karibuni kumesambazwa qiraa yenye mvuto ya Qur'ani Tukufu ya qarii maarufu wa Misri Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar.

Qiraa hii imetajwa kuwa ni ya mwaka 2016 nchini Misri.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Afrika Kusini, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3923873

 

captcha