IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Meshkat

Usajili wa Mashindano ya 3 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat

15:44 - December 31, 2023
Habari ID: 3478122
IQNA – Usajili umeanza kwa ajili ya Toleo la Tatu la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat, ambayo hufanyika mtandaoni chini ya usimamizi wa Taasisi ya Qur'ani ya Meshkat.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa taasisi hiyo Hujjatul Islam Mojtaba Mohammadi alipokuwa akitangaza maelezo kamili ya mashindano hayo katika  kikao na wanahabari siku ya Jumamosi.

Mashindano hayo yana kategoria mbili: Usomaji wa Qur'ani Tukufu kwa mbinu ya Taqlid kwa wanaume na kuhifadhi Qur'ani Tukufu  kwa wanaume na wanawake.

Kategoria ya kisomo inawahitaji washiriki kuiga mojawapo ya visomo vinne vilivyochaguliwa vya maqari mashuhuri ambao ni  Sheikh Mohamed Siddiq El-Minshawi, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, Sheikh Shahat Muhammad Anwar, na Sheikh Mustafa Ismail.

Ushindani uko wazi kwa waombaji kutoka kote ulimwenguni, lakini fainali ni mshiriki mmoja tu kutoka kila nchi atachaguliwa.

Hatua ya mwisho itafanyika katika Haram ya Imam Ridha AS huko Mashhad mnamo Januari 6-7.

Tarehe ya mwisho ya usajili ni Januari 20, na wagombea wanaotaka kushuriki wanaweza kutuma maombi kupitia tovuti  hii ya Taasisi ya Qur'ani ya Meshkat.

Washindi wa kila kategoria watapata zawadi ya pesa taslimu karibu USD 2,000, huku watakaoshika nafasi za pili wakitazamiwa kupata karibu USD 1,600 na USD 1,400 mtawalia.

Toleo la awali la shindano hilo lililofanyika mwaka jana, lilivutia washiriki zaidi ya 1,000 kutoka nchi 73, kati yao 153 walifanikiwa kuingia hatua ya fainali.

4190864

Habari zinazohusiana
captcha