IQNA

Turathi ya Kiislamu

Nakala ya Msahafu wa kale wa Mashhad yazawadiwa Haram ya Imam Hussein (AS)

15:51 - December 09, 2023
Habari ID: 3478012
KARBALA (IQNA) – Kopi ya nakala ya kodexi ya Msahahafu wa karne 14 zilizopita wa Mashhad, (Mus'haf Mashhad Razawi) imekabidhiwa Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq.

Mtafiti na mfasiri wa Qur'ani Tukufu  Morteza Kariminia alitoa alikabidhi kopi ya Msahafu huo kwa Isa al-Kharsan, afisa idara hiyo wiki iliyopita..

Msahafu huo umeandikwa kwa maandishi ya Hijazi - jina la pamoja la idadi ya maandishi ya awali ya Kiarabu ambayo yalikuzwa katika eneo la Hejaz la Arabia.

Kariminia amebainisha kuwa Taasisi ya Aal-Bayt iliyoko Qom, Iran kwa kushirikiana na Astan Quds Razavi (Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS)-), imechapisha maandishi kamili ya Msahafu huo wa Mashhad.

Kopi ya Msahafu huo inajumuisha maelezo na utangulizi katika lugha la Kiarabu na Kiingereza, zilizowasilishwa ili kufikisha ujumbe kamili.

Msahafu huo ulizinduliwa Mashhad mwezi uliopita na una kurasa 252 na asilimia 95 ya maandishi ya Qur'ani Tukufu.

Msahafu huo uliandikwa kwenye ngozi yenye ukubwa wa sentimeta 35 kwa 50 ima Madina au Kufa na baadaye ikapelekwa Khorasan (kaskazini mashariki mwa Iran).

Kisha mwishoni mwa karne ya 5 Hijria, mmiliki aliukabidhi Msahafu huo kama zawadi kwa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad katika eneo hilo la Khorassan.

Habari zinazohusiana
captcha