IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran asisitiza haki ya nyuklia ya Iran

22:15 - April 08, 2022
Habari ID: 3475101
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesisitiza kuwa sekta ya nyuklia ni haki ya kidini na kisheria ya wananchi wa Iran.

Katika hotuba za Sala ya Ijumaa leo iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Kadhim Seddiqi ameashiria "Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia" na kueleza kuwa: Nishati ya nyuklia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya dunia ya sasa katika nyanja za kitiba, madawa na kusafisha maji chumvi. Seddiqi ameongeza kuwa: Wananchi wa Iran wanaihitajia sekta hiyo; kwa hiyo ni haki ya kidini na kisheria ya watu wa Iran kunufaikka na sekta hiyo.  

Kuhusu kuendelea mazungumzo ya JCPOA, Imam wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi anasisitiza kuwa, Iran haina imani na pande zingine katika maungumzo hayo na kwamba inataka kupewa dhamana inayohitajika na hakikisho la kivitendo. 

Hujjatul Islam Walmuslimin Kadhim Seddiqi amebainisha kuwa: Serikali inafanya juhudi za kuondola kamilifu  vikwazo dhidi ya nchi hii.  

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Imam wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria tukio lililojiri katika mji wa Mash'had na kueleza kuwa: Wanazuoni wawili wameuliwa shahidi katika mwezi wa Mwenyezi Mungu, mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakiwa katika Haramu Tukufu ya Imam Ridha AS;  kuuliwa kwao shahidi ni karama, hadhi na utukufu waliotunukiwa na Mola Karima. 

Jumanne alasiri mtu mmoja mwenye fikra potofu za kitakfiri aliwashambulia kwa kisu wanazuoni watatu waliokuwa wamekwenda kufanya ziara katika Haramu ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW,, Imam Ridha AS, katika mji wa Mashhad ulioko Kaskazini Mashariki mwa Iran na kuwauwa shahidi wawili miongoni mwao na kumjeruhi mmoja.  

Mtenda jinai hiyo alikamatwa na maafisa usalama na tayari amekabidhiwa kwa vyombo vya usalama vya Iran. 

4047657

captcha