IQNA

Misikiti, Makanisa kutumika Kenya katika zoezi la chanjo ya COVID-19

16:38 - January 04, 2022
Habari ID: 3474765
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Kenya imeazimia kushirikiana na misikiti pamoja na makanisa nchini humo ili kuongeza idadi ya wale wanaodungwa chanjo ya COVID-19 nchini humo.

Mapema Disemba 2021, Wizara ya Afya ya Kenya ilitangaza kuanza ushirikiano wake na misikiti pamoja na makanisa ili maeneo hayo ya ibada yatumike kama vituo vya kuwadunga waumini chanjo ya COVID-19.

Hadi kufikia Disemba 31 2021, dozi milioni 9.8 za COVID-19 zilikuwa zimetolewa kote Kenya ambapo watu milioni 5.7 walikuwa wamepokea dozi moja na wengine milioni 4.08 walikuwa wamepokea dozi moja.

Hadi sasa ni wasilimia 15 tu ya watu wazima ndio waliochanjwa nchini Kenya na serikali ya nchi hiyo inapanga kuhakikisha kuwa watu milioni 27 wanapokea chanjo mwisho wa mwaka huu wa 2022.

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa kila mtu anayetakahuduma za serikalini sharti awe amepokea chanjo kwa ukamilifu . Aidha watu wanaotaka  usafiri wa umma  na kuingia maeneo mengine ya umma kama vile benki na maduka ni sharti wathibitishe kupata chanjo kikamilifu. 

/4025098

captcha