Makamanda wa kijeshi wameiambia SNA Radio kwamba, viongozi watatu wa magaidi hao wakufurishaji wa al Shabab ni miongoni mwa waliouawa kwenye operesheni zilizopfanyika katika vijiji vya Busley na Bulo Alundi katika eneo la Janale la jimbo hilo la Shabelle.
Mamakanda wa Jeshi la Taifa la Somalia wamesema kuwa, magaidi wengine kadhaa wamejeruhiwa na maficho yao yameteketezwa katika operesheni hizo zilizofanyika baada ya makachero wa jeshi hilo kugundua maficho ya magaidi hao.
Maafisa hao wa Jeshi la Taifa la Somalia pia wamesema, ulinzi utaimarishwa na operesheni zitaongezwa katika eneo hilo hadi magaidi wote wa al Shabab watakaposafishwa. Jimbo la Shabelle ni katika maeneo ambayo yanatumiwa sana na magaidi wa al Shabab kufanya mashambulizi huko kusini mwa Somalia.