IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na Waziri Mkuu wa Iraq

17:43 - July 19, 2020
Habari ID: 3472978
TEHRAN (IQNA) – Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko mjini Baghdad leo amekutana na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi.

Kwa mujibu wa taarifa wamejadili masuala kuhusu uhusiano wa nchi mbili na safari tarajiwa ya waziri mkuu wa Iraq nchini Iraq. Aidha wamebadilishana maoni kuhusiana na matukio ya kieneo na kimataifa.

Mapema leo Zarif alisema Jamhuri ya Kiislamu na Iraq daima zinapaswa kuwa macho na tayari kwa ajili ya kukabiliana na njama za magenge ya kigaidi kama vile Daesh (ISIS) katika eneo hili la Asia Magharibi.

Zarif amesema hayo katika kikao na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Iraq, Fuad Hussein.

Amesema ingawaje eneo hili lilipata pigo kubwa baada ya Marekani kuwaua kigaidi Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na aliyekuwa Naibu Mkuu wa harakati ya wananchi ya Hashdu Shaabi ya Iraq,  Abu Mahdi al-Muhandis, lakini nchi mbili hizi jirani zitaendelea kushirikiana katika vita dhidi ya magenge ya kigaidi.

Dakta Zarif ambaye baada ya kuwasili Iraq ametembelea eneo walipouawa shahidi makamanda hao wa Iran na Iraq amesisitiza kuwa, Tehran na Baghdad zinafanya jitihada za pamoja za kuhakikisha kuwa wahusika wa jinai hiyo ya kigaidi wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Huku akishiria kuwa uhusiano wa Tehran na Baghdad umejengeka katika misingi ya udugu, urafiki na kuheshimiana, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema nchi mbili hizi zina azma ya kuimarisha uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara, licha ya janga la corona.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein kwa upande wake amesema katika mazungumzo yake na Dakta Zarif kuwa wamegusia umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyuga za biashara, utalii wa kidini, nishati na njia za baharini na reli.

3911337

captcha