IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Maqari wa Algeria, Malaysia, na Indonesia washinda mashindano ya Qur’ani Qatar

0:04 - April 07, 2024
Habari ID: 3478642
IQNA - Washindi wa  mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yajulikanayo kama Tuzo ya Kuhifadhi Qur'ani ya Katara 2024 walitunukiwa katika hafla iliyofanyika Doha, Qatar, Ijumaa.

Taasisi ya Cultural Village Foundation (Katara) ilitangaza walioshika nafasi tatu za juu katika hafla hiyo.

Yassin Amran kutoka Algeria alijinyakulia zawadi ya kwanza yenye thamani ya QR 500,000, wakati zawadi ya pili ilikwenda kwa Mohamed Husseini Mahmor kutoka Malaysia, yenye thamani ya QR 300,000. Zawadi ya tatu ilitolewa kwa Mohamed Fuji Ridwan kutoka Indonesia, yenye thamani ya QR 100,000.

Akizungumza katika hafla hiyo,  Meneja Mkuu wa Katara, Dk. Khalid bin Ibrahim Al Sulaiti, alitoa shukurani za dhati kwa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu, mdhamini rasmi wa Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur'ani kwa uungaji mkono wao endelevu, ambao umeipandisha tuzo hiyo kufikia hadhi mashuhuri kimataifa.

Pia alitoa shukrani zake za dhati kwa Televisheni ya Qatar, mshirika wa vyombo vya habari wa tuzo hiyo, kwa kupanua wigo wa Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur'ani kwa kutangaza mashindano hayo katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wajumbe wa kamati ya majaji wa Tuzo ya Kuhifadhi Qur'ani ya Katara, katika kategoria za Tajwid na utendaji wa sauti, wamesisitiza kuwa toleo hili la tuzo hiyo lilibainishwa na tafauti za washiriki kutoka takriban nchi 64 duniani, na hivyo kuimarisha anga yake ya ushindani.

Wakati huohuo, washindi wa Tuzo ya Kuhifadhi Qur'ani ya Katara walieleza furaha yao kwa kupokea tuzo hiyo maarufu duniani, wakibainisha shirika lake la kipekee na washiriki mbalimbali kutoka mabara yote.

 

 

Algerian, Malaysian, Indonesian Qaris Win Katara Quran Award in Qatar

Algerian, Malaysian, Indonesian Qaris Win Katara Quran Award in Qatar

Algerian, Malaysian, Indonesian Qaris Win Katara Quran Award in Qatar

 

 

3487818

captcha