Huu ulikuwa ni mwaka wa sita mfululizo ambapo mashindano ya Qur'ani yalifanyika Jakarta, mji mkuu.
Mkuu wa tawi la idara hiyo mjini Jakarta Dk Abdullah Beik alisema: "Tunasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Mtume wa Rehema kwa muda wa mwezi mzima katika miji tofauti ya Indonesia. Kama sehemu ya maadhimisho haya, tawi letu liliamua kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, chini ya usimamizi wa na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS)."
Aliongeza, “Zaidi ya washiriki 200 wa kike na kiume walishiriki katika shindano hilo, ambalo lilifanyika katika ofisi yetu huko Jakarta.”
3485770