TEHRAN (IQNA) – Qari wa kimataifa wa Iran Alireza Bijani hivi karibuni amesoma aya za 63 hadi 71 za Surah Al-Furqan katika Qur'ani Tukufu.
Hapa chini ni tarjama ya aya hizo:
- Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!
- Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.
- Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi.
- Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya.
- Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.
- Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara,
- Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.
- Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
- Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.