IQNA

Mshikamano wa Sauti ya Waislamu wa Afrika Kusini kwa Palestina

17:18 - October 09, 2023
Habari ID: 3477701
CAPE TOWN (IQNA) - Jumuiya ya Waislamu huko Cape Town, Afrika Kusini ilifanya mkutano ili kutoa msaada na ushirikiano kwa watu wa Palestina.

Walikusanyika katika msikiti wa Al Quds wa mji huo kwa mshikamano na Wapalestina siku ya Jumapili.

Harakati za ukombozi za Afrika Kusini "pia zililazimishwa kuchukua silaha ili kuwa na athari, alisema Shaykh Shahid Esau, mbunge wa zamani wa bunge la Afrika Kusini.

Wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi, "jumuiya ya ulimwengu iliitwa kuweka vikwazo dhidi ya Afrika Kusini na tunapata nchi zile zile za Magharibi ambazo ziliunga mkono Afrika Kusini wakati wa utawala wa kibaguzi  ni watu wale wale ambao sasa wanaiunga mkono Israeli dhidi ya Wapalestina,aliongeza kwa kusema;

Taasisi ya Al Quds (SA) pia iliandaa misa ya Khatam al Qu’rani Tukufu  (kusoma Qur'ani nzima) kwa ajili ya kuwakomboa Wapalestina wanaodhulumiwa katika msikiti huo.

Sheikh wa Baraza la Mahakama ya Kiislamu (MJC) Sheikh Ebrahim Gabriels na Moulana Abdul Khaliq Allie walihutubia umati juu ya lengo la mkutano huo.

Hayo yanajiri wakati utawala wa Israeli ukiushambulia Ukanda wa Gaza uliokaliwa kwa mabavu  uliozingirwa kwa usiku wa pili mfululizo baada ya kutangaza rasmi vita dhidi ya kundi la Hamas la Palestina, Jeshi lake linasema kuwa wanajeshi 100,000 wa akiba wamejikusanya karibu na Gaza.

Operesheni Al-Aqsa Mafuriko ‘Sura Mpya’ katika Makabiliano dhidi ya Ukaliaji; Hamas

Mapigano makali yanaendelea kati ya wapiganaji wa Kipalestina na wanajeshi wa Israeli katika maeneo matatu katika maeneo ya kusini ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, ikiwemo kibbutz huko Karmia na katika miji ya Ashkelon na Sderot.

Idadi ya hivi punde ya vifo imefikia Wapalestina 413, kulingana na maafisa wa afya, na zaidi ya Waisraeli 700, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Hamas na Palestina Islamic Jihad walisema wanawashikilia zaidi ya watu 130 mateka ndani ya Gaza.

Operesheni ya kushtukiza ya Hamas, operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa, ilikuja baada ya walowezi wa Kiisraeli kuvamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika siku za hivi karibuni na idadi kubwa ya Wapalestina waliuawa na Israeli katika miezi ya hivi karibuni.

 

3485488

captcha