IQNA

Wananchi wa Iran washerehekea ushindi wa kihistoria wa Wapalestina

11:40 - October 08, 2023
Habari ID: 3477700
TEHRAN (IQNA) –Wananchi wa jiji la Tehran wamekusanyika mbele ya ubalozi wa Palestina kusherehekea ushindi wa kihistoria waliopata wanapambano wa Palestina katika shambulio kubwa walilofanya jana Jumamosi dhidi ya Wazayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, wananchi na wanafunzi wa vyuo vikuu walikusanyika jioni ya jana mbele ya ubalozi wa Palestina hapa mjini Tehran na kusherehekea ushindi huo.

Wananchi hao wamesikika wakisema kwa sauti kubwa: "Mauti kwa Israel!" "Mauti kwa Marekani!" Allahu Akbar! Allahu Akbar! Labayka ya Aqsa! Labaika ya Falastin! Labaika ya Khamenei! 

Watu waliokusanyika kwenye sherehe hizo wamebeba bendera za Palestina na picha za Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambaye aliuliwa shihidi kidhulma na Wamarekani alipokuwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq, mjini Baghdad, tarehe 3 Januari, 2020.

Ismail Hania, Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliposhiriki kwenye maziko ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, alitangaza rasmi kuwa mwanamapambano huyo ni shahidi wa Quds na ameuawa katika njia ya kuupigania Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Wapalestina jana Jumamosi walifanya operesheni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi dhidi ya Israel, ya mashambulio ya kushtukiza ambayo yamefanywa na wanamapambano waliovuka uzio na kuingia katika miji inayokaliwa kwa mabavu, sambamba na msururu mkubwa wa maroketi yaliyovurumishwa kutokea Ukanda wa Ghaza.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimewaonesha wanamapambano wa Muqawama wakiwa ndani ya kambi ya kijeshi jana, huku miili ya wanajeshi wa Kizayuni walioangamizwa ikiwa imezagaa huku na kule.

Tawi la kijeshi la Hamas Izzuddin al Qassam lilitangaza jana kuwa, zaidi ya makombora 7,000 yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza mapema jana kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, na kutangaza kuwa limeanzisha "Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa."

 

4173633

 

 

captcha