IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah:

Lengo la kuvunjia heshima Qur'ani ni kuibua fitina baina ya Waislamu na Wakristo

16:23 - July 13, 2023
Habari ID: 3477276
BEIRUT (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, lengo la kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kutaka kuzusha hitilafu baina ya Waislamu na Wakristo.

Seyyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa muqawama katika vita vya siku 33 na kubainisha kwamba, mtu aliyechoma nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Uswidi ana uhusiano na Shirika la Kijasusi la Israel (MOSSAD).

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Waislamu na Wakristo wanapaswa kujitokeza na kuzuia vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na kushirikiana kwa ajili ya kuzima moto huu wa fitina

Katika upande mwingine, kiongozi huyo wa Hizbullah ya Lebanon sambamba na kueleza kuwa, Wazayuni na Wamarekani wamekiri mara chungu nzima juu ya kushindwa kwao katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006 amesema, lengo hasa la vita hivyo lilikuwa ni kuuangamiza muqawama wa Lebanon na kuilazimisha nchi hiyo isalimu amri mbele ya masharti ya utawala ghasibu wa Israel na Marekani mkabala na muundo mpya wa eneo.

Kadhalika Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, ushindi wa kambi ya muqawama katika vita vya siku 33 mwaka 2006 uliiweka pabaya Israel na kuifanya ielekee katika mkondo wa kusambaratika.

3484327

captcha