Katibu wa Makao Makuu kwa ajili ya kuadhimisha miaka mitatu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Soleimani, Hujjatul Islam Mohammad Reza Shafiei, alisema msafara huo unajumuisha baadhi ya wasomaji mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran
Msafara huo utakuwa na vikao vya Qur'ani Tukufu katika miji kadhaa ya Iran, ikiwa ni pamoja na Tehran, Yazd, Kashan, Naeen, Ardakan, na Kerman, alibainisha.
Ameongeza kuwa, msafara huo utawasili Kerman siku ya Jumamosi ili kushikilia duru ya Qur'ani na kusoma Fatiha kwenye kaburi la Shahidi Soleimani mkoani humo
Jeshi la Marekani liliwaua kigaidi Jenerali Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa Hashd Al-Shaabi au Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (PMF) waliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo Januari 3, 2020. Shambulizi hilo liliamriwa moja kwa moja na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Vikao mbalimbali vimepangwa kuandaliwa nchini Iran, Iraq na nchi nyingine kadhaa ili kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Jenerali Soleimani, al-Muhandis na wanamapambano waliokuwa wameandamana nao.
4110465