IQNA

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Ayatullah Sistani atoa rambirambi kwa kifo cha Ayatullah Rouhani

15:55 - December 17, 2022
Habari ID: 3476262
TEHRAN (IQNA) – Kufuatia kifo cha Faqihi mashuhuri wa madhehebu ya Shia Ayatullah Mohammad Sadeq Rouhani, Marjaa Taqlid wa Iraq Ayatullah Seyed Ali al-Sistani alitoa ujumbe wa rambirambi siku ya Jumamosi.

Katika ujumbe wake, Ayatullah Sistani alimsifu marehemu mwanazuoni huyo kwa kutumia miaka mingi ya maisha yake katika kuwafundisha na kuwafunza wanafunzi wa seminari na kuendeleza mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS).

Alitoa salamu za rambirambi kwa Imam Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Vyuo Vikuu vya Kiislamu (Hauza) katika mji wa Qom nchini Iranna wanafamilia na wafuasi wa Ayatullah Rouhani.

Ayatullah Sistani pia alimuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake rehema na ainue safu yake na kuwapa subira familia iliyofiwa.

Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani, mmoja wa wanazuoni wa Chuo cha Kidini cha Qom, ameaga dunia usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, ofisi ya Ayatullah Rouhani imetoa tangazo ikieleza kwamba: Magharibi ya Ijumaa ya jana, Desemba 16, 2022, roho tukufu na iliyotukuka ya Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani imeungana na mababu zake watoharifu.

Alimu huyo alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Ayatullahil-Udhma Khoui (RahamtuLlahi-Alayhi) na alifikia daraja ya kielimu ya Ijtihad akiwa na umri wa miaka 14 kwa kuthibitishwa kimaandishi ya walimu wake.

Ayatullah Seyyed Muhammad Sadiq Rouhani amealifu vitabu kadha wa kadha kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi, mojawapo ya vilivyo muhimu zaidi kikiwa ni kitabu kiitwacho Fiqhu-Sadiq.

Mwanazuoni huyo alizaliwa katika mwezi wa Mfunguo Nne, Muharram 1345 mwaka wa mwandamo wa Hijria katika mji mtukufu wa Qom.

4107583

captcha