Akizungumza katika mkutano na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Lebanon Seyed Komeyl Baqerzadeh, Sheikh Jabri alisema Iran ni mwanachama wa juu wa mhimili wa upinzani.
Kwa kuzingatia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran inakabiliana na vitisho kwa muqawama na kusimama kidete.
Sheikh Jabri pia alisifu mafanikio na ushindi wa Iran dhidi ya madora yenye kiburi au ya kiistikbaru duniani, Uzayuni na tawala zinazopinga mabadiliko.
Katika mkutano huo, afisa huyo wa Iran na mwanasiasa huyo wa Lebanon walijadili maendeleo ya kieneo na masuala ya kiutamaduni na kiakili.
Walisisitiza haja ya juhudi za kufikia malengo ya pamoja ya Kiislamu, hasa katika masuala ya kuendeleza mafundisho ya Uislamu.
Walisema hili lifanyike kwa kuzingatia umoja na kuamurisha mema na kukataza maovu.
Mhimili wa Muqawama unajumuisha Iran, Syria, na harakati za mapambano hasa Hizbullah, Hamas, Jihad Islami, Ansarullah na makundi mengine ya muqawama katika eneo.
4085202