IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya watoto Wapalestina mjini Quds

13:59 - November 11, 2021
Habari ID: 3474543
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya watoto Wapalestina yameanza Jumatano katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi.

Idara ya Wakfu ya Palestina na Wizara ya Masuala ya Kidini ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeandaa mashindano hayo kwa kushirikiana na Banki ya Safa.

Mashidano hayo ni ya kuhifadhi Juzuu sita za Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi walio katika umri wa baina ya miaka 6 hadi 18.

Naibu Waziri wa Masuala ya Kidini Palestina Hisham Abu al Rub amesema mashindano hayo ya Qur'ani yanalenga kuwahimizha wanafunzi Wapalestina wahifadhi Qur'ani na kujifunza Uislamu. Wanafunzi 3000 wanashiriki katika mashindano hayo.

4012358

captcha