IQNA

Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Lebanon ameaga dunia

20:51 - March 03, 2021
Habari ID: 3473700
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Lebanon, Sheikh Ahmed al-Zein, ameaga dunia Jumanne.

Sheikh al-Zein ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Wanazuoni Waislamu Lebanon na pia alikuwa miongoni mwa wanazuoni maarufu wa Ahlu Sunna nchini humo.

Aidha Sheikh al Zein ambaye aliwahi kuwa jaji au kadhi katika mahakama ya mji wa Sidon Lebanon ni maarufu kwa misimamo yake imara dhidi ya utawala wa Kizayuni na alisisitiza kuwa mapambano ni njia pekee ya kuuangamiza utawala huo.

Halikadhalika aliitambua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mbeba bendera ya mapambano na ukombizi Palestina na mji wa Quds.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa na kubainisha masikitiko yake makubwa kutokana na kuaga dunia mwanazuoni huyo baada ya maisha ya jihadi na elimu.

3957257

Kishikizo: lebanon ahmed al zein
captcha