IQNA

Tizama Qiraa ya Qur’ani ya Shahat Anwar katika Mwezi wa Ramadhani- Video

13:29 - May 11, 2020
Habari ID: 3472757
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Shahat Mohammad Anwar amesoma aya 185 ya Sura Al-Baqara kuhusu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Sawmu pamoja na aya ya 186 ya sura hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya youm7, Sheikh Shahat Mohammad Anwar ambaye ni kati ya wasomaji Qur’ani (qarii) mashuhuri Misri na ulimwengu wa Kiislamu alizaliwa 29 Mei mwaka 1978 katika eneo la Mit Ghamr  mkoani El Dakahila nchini Misri.

Akiwa bado mototo mdogo alihifadhi Qur’ani Tukufu kwa msaada wa baba yake na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Al Azhar na kuhitimu katika taalauma ya fasihi ya Kiarabu.

Qarii huyu kijana kutoka Misri mnamo mwaka 2004 alipita mtihani na kuweza kuidhinishwa kuwa qarii rasmi wa Radio ya Misri.

3897998

captcha