IQNA

Vipindi vya Qur'ani katika TV ya Uganda

14:57 - June 09, 2015
Habari ID: 3312613
Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Kampala, Uganda kinashirikiana na Televisheni ya kitaifa ya nchi hiyo UBC TV katika kutayarisha pamoja vipindi vya Qur'ani na vya maudhui za kidini.

Vipindi hivyo vinatazamiwa kurushwa hewani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu kuanzia Juni 18 hadi Julai 17.
Uamuzi huo umechukuliwa katika kikao baina ya mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Iran mjini Kampala Ali Bakhtiari na maafisa waandamizi wa UBC TV.
Katika kikao hicho, Bakhtiari ameitaja Qur'ani Tukufu kuwa Neno la Allah SWT na kwamba  Qur'ani Tukufu inatoa wito wa amani na urafiki baina ya mataifa. Aidha amesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa harakati za Qur'ani katika jamii.
Ameongeza kuwa Kituo cha Utamaduni cha Iran kiko tayari kushirikiana zaidi na UBC TV katika kutayarisha vipindi zaidi vya Qur'ani, kidini, kiutamaduni na katika uga wa mahusiano baina ya wafuasi wa duni mbali mbali.
Wakuu wa UBC TV wametangaza azma yao ya kushirikiana na kituo hicho cha Iran.

captcha