IQNA

Waislamu Cuba wataka msikiti mjini Havana

11:57 - February 21, 2015
Habari ID: 2877957
Waislamu nchini Cuba wametoa wito wa kujengwa msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo, Havana.

Kwa mujibu  wa mwandishi wa IQNA, Waislamu nchini Cuba wamesema ni jambo lisilokubalika kwa mji mkuu wa nchi hiyo kutokuwa na Msikiti. Kutokanana kukosekana msikiti, Waislamu mjini  Havana huswali sala ya Ijumaa katika  jengo lijulikanalo kama Baitul Arabi (Nyumba ya Kiarabu) katika eneo la kale mjini humo.
Mwezi Novemba mwaka jana serikali ya Cuba ilitangaza kutoa eneo kwa shabaha ya kujengwa msikiti wa kwanza nchini humo, utakaojengwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Havana. Viongozi wa serikali ya Cuba wameeleza kuwa, ardhi hiyo yenye ukubwa wa ekari tano iko katika eneo la mji mkongwe wa Havana, imetengwa rasmi kwa ajili ya kujengwa msikiti na shughuli nyingine zinazohusiana na wafuasi wa dini ya Kiislamu. Imeelezwa kuwa, mchoro wa ujenzi wa msikiti huo utafanana na Masjidul Ortakoy ulioko Istanbul nchini Uturuki. Viongozi wa serikali ya Cuba wameeleza matumaini yao kwamba, nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC zitafanya juhudi maradufu za kuhakikisha ujenzi wa msikiti huo unakamilika, na kuwaondolea kero Waislamu wa nchini humo.../mh

2876899

captcha