IQNA

Sayyid Nasrallah

Marekani haina ustahiki wa kupambana na ugaidi

12:54 - September 27, 2014
Habari ID: 1454360
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa Marekani haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo kupitia hotuba aliyoitoa jana usiku.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria juhudi zinazodaiwa kufanywa na Marekani kwa ajili ya kuasisi muungano dhidi ya Daesh na kusisitiza kwamba Hizbullah inalipinga kundi la Daesh na mirengo yote ya kitakfiri na yenye kushupalia vita na kwamba harakati hiyo inapambana na makundi hayo. Amesema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon iko tayari kuendesha mapambano dhidi ya makundi ambayo yanaua wananchi na kuwatishia raia na mataifa ya eneo hili. Sayyid Hassan Nasrullah aliongeza kama ninavyomnukuu" msimamo wetu kuhusiana na muungano wa kimataifa hauna uhusiano wowote na msimamo wetu kuhusiana na Daesh, kimsingi sisi tunapinga muungano wa kimataifa amma uwe dhidi ya Syria au dhidi ya Daesh au kinyume chake; na msimamo wetu haubadiliki kuhusiana na suala hilo na hatutakubali Lebanon iwe sehemu ya muungano huo wa kimataifa". Mwisho wa kunukuu. Nasrulllah amekumbusha kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha ugaidi na muungaji mkono wa suala hilo na muungaji mkono pia wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema Marekani ilikuwa na nafasi kuu katika kuasisiwa makundi ya kigaidi na haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesisitiza kuwa, kama alivyosema mara kadhaa Rais wa Marekani Barack Obama kwamba muungano huo ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya Marekani, hivyo wao hawana maslahi yoyote na muungano huo.

mh1453351

Kishikizo: lebanon hizbullah daesh
captcha