IQNA

Abdul-Malik Badreddin al-Houthi

Marekani iliiamuru Saudi Arabia iishambulie Yemen

17:46 - September 21, 2016
Habari ID: 3470574
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema Marekani ndiyo iliyotoa amri ya kushambuliwa nchi hiyo.

Abdul-Malik Badreddin al-Houthi ameyasema hayo mjini Sanaa mji mkuu wa Yemen kwa mnasaba wa sherehe yaGhadir Khum inayokumbushia tukio la kihistoria la kutangazwa na Mtume (saw) Imam Ali Bin Abi Twalib (as) kuwa kiongozi wa Waislamu baada yake na kuongeza kuwa, ni mwaka mmoja na nusu umepita ambapo raia wa Yemen wanashuhudia mauaji ya kutisha yanayofanywa na Saudia. Amesema utawala wa Saudia ni wa kikatili na usio na huruma hata chembe.

Akiashiria kuwa, Saudia inatekeleza siasa za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, amewataka Wayemen na Umma wa Kiislamu kwa ujumla kupambana na njama chafu za Marekani na utawala wa Aal-Saud.Ameongeza kwamba, Marekani ndiyo iliyotoa amri ya kutekelezwa mashambulizi hayo na kwamba ni nchi hiyo hiyo inayoyasimamia. AidhaKatibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu nchini Yemen amesema kuwa, Marekani na Saudia zilianzisha hujuma hizo nchini Yemen bila kuwepo sababu yoyote muhimu na kwamba hadi sasa wametekeleza mauaji ya umati dhidi ya Wayemen wasio na hatia. Hata hivyo amesisitiza kwa kusema kama ninavyomnukuu: "Ni lazima tutekeleze wadhifa wetu. Matakwa yetu yapo wazi na hayajafichika kwa yeyote." Mwisho wa kunukuu.

Aidha amesema kuwa, pamoja na matatizo chungu nzima yanayolikabili taifa hilo, lakini hadi sasa Wayemen wameendelea kuwa kitu kimoja na kwamba umoja unaweza kukabiliana na changamoto ya kijeshi au ya kiuchumi. Amesema kuwa, lengo la utawala wa Saudia katika kushirikiana na maadui wa Kiislamu ni kujaribu kuwafanyaWaislamu kuachana na matukufu yao ya kidini kwa kuifuata Marekani, Israel na marafiki wao.

Tangu ulipoanzisha uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya Yemen mnamo mwezi Machi mwaka uliopita, hadi sasa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud na kuungwa mkono na Marekani umesha zishambulia skuli, hospitali, maeneo ya makaazi ya raia, barabara, masoko na kambi za wakimbizi na kuua maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Zaidi ya watu 10,000 wamepoteza maisha katika hujuma ya kinyama ya Saudia dhidi ya Yemen.

Lengo kuu la hujuma ya Saudia kuihujumu Yemen ni kumrejesha madarakani kibaraka wake, Rais mtoro wa nchi hiyo aliyejiuzulu Abd Rabu Mansour Hadi na kuwaondoa madarakani wanamapinduzi wa Ansarullah.

3460969

captcha