IQNA

Elimu

Mkuu wa Al-Azhar asisitiza tarjuma sahihi ya maandiko ya Kiislamu

17:23 - April 25, 2024
Habari ID: 3478733
IQNA - Rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri ameisitiza haja ya kulipa kipaumbele maalum  suala la tarjuma au tafsiri sahihi ya maandishi ya Kiislamu

Akihutubia mkutano wa “teknolojia, tarjuma, na ufundishaji wa lugha; matarajio na changamoto”, Sheikh Salama Dawood alisema kukosekana kwa usahihi katika kutafsiri maandishi ya Kiislamu kunaweza kusababisha kupotoshwa kwa taswira ya Uislamu, kanuni zake na ufahamu wake, tovuti ya Al-Liwa iliripoti.

Pia alisema tafsiri ni njia ya kufikisha utamaduni na mawazo kwa lugha mbalimbali. Dawood alibainisha kuwa nchi za Magharibi zimepata maendeleo yake kutokana na tafsiri ya sayansi ya Kiislamu na turathi za kiakili.

Pia naibu wa Al-Azhar Sheikh Mohamed al-Duwaini alizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mjini Cairo.

Ameashiria kukua kwa chuki dhidi ya Uislamu duniani katika miaka ya hivi karibuni na kueleza kuwa ni jambo linalotaka kuudhoofisha Uislamu na kueneza chuki dhidi ya Uislamu.

Amesema wanaochunguza jambo hilo wanajua vyema kwamba kukosekana kwa usahihi katika kufasiri matini za Kiislamu na kufikisha mafundisho na fikra za Kiislamu kwa nchi za Magharibi kumechangia uzushi.

4212257

Kishikizo: misri al azhar tarjuma
captcha