IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu Ufaransa

Shule mbili za Kiislamu zafungwa Kusini mwa Ufaransa

12:57 - November 18, 2022
Habari ID: 3476108
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Ufaransa wameifunga shule mbili za Kiislamu katika mji wa kusini wa Montpellier, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Maafisa walifanya ukaguzi wa kushtukiza katika shule hizo mbili mnamo Jumanne na kuamuru wasimamizi kuzifunga.

Uvamizi huo ulitekelezwa kwa maagizo ya Hugues Moutouh, gavana wa eneo la Herault.

Msikiti mdogo katika mojawapo ya shule pia utafungwa.

Kulingana na Moutouh, shule hizo zilikuwa "zinaendeshwa kinyume cha sheria" na msikiti ulikuwa ukifanya kazi bila ruhusa, ripoti hiyo ilisema.

Sheria mpya yenye utata iliyoanzishwa nchini Ufaransa mwaka jana imekosolewa kwa kulenga kuwatenga na kuwakandamiza Waislamu, huku baadhi ya misikiti 25 ikiwa imefungwa nchini humo kwa visingizio mbalimbali hivi karibuni

Ripoti ya chuki dhidi ya Uislamu ya Ulaya 2021 iliyotolewa miezi michache iliyopita ilisema sheria hiyo mpya "ambayo inapaswa kutoa jibu kali dhidi ya 'ugaidi' na 'Uislamu wenye itikadi kali', kwa kweli imechochea ukandamizaji mkali dhidi ya Waislamu na taasisi za Kiislamu.

Ripoti hiyo ilibainisha Ufaransa kama mojawapo ya "maeneo makuu ya chuki dhidi ya Waislamu na matukio ya chuki ya Uislamu" katika bara hilo.

"Sera ya chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia nchini Ufaransa kimsingi inatakelezwa na kusimamiwa na serikali, ambayo inataka kuanzisha 'Uislamu wa Ufaransa' ambao unaawazuia Waislamu kujisimamia mambo yao huku lengo likiwa ni  kuwafanya Waislamu wa Ufaransa kuwa 'Waislamu bila Uislamu'," ilisoma ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ilibaini kuwa mwaka 2021 kulishuhudiwa "kiwango cha juu zaidi cha vurugu nchini Ufaransa ambapo matamshi ya  chuki dhidi ya Uislamu yaliongezeka sambamba na kutekelezwa sheria zinazowakandamiza Waislamu kidini na hivyo kuwafanya Waislamu wa Ufaransa kuwa raia wa daraja la pili katika nchi yao.

3481296

captcha