IQNA

Wasomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu / 10

Muhammad Abdul Aziz Hassan; Qari aliyekumbatia mitindo ya zamani na ya kisasa ya qiraa

17:16 - November 17, 2022
Habari ID: 3476105
TEHRAN (IQNA) - Misri imeweza kuibua wasomaji wengi mashuhuri wa Qur’ani ambao wamevuma katika ulimwengu wa Kiislamu. Mmoja wao ni Sheikh Muhammad Abdul Aziz Hassan, qari ambaye aliweza kuingiza mitindo ya zamani na ya kisasa na kuunda mtindo wake wa qiraa ya Qur'ani Tukufu kusoma.

Ustadh Hassan aliingia katika redio ya taifa ya Misri kama msomaji wa Qur'ani mwaka wa 1964 na tangu wakati huo alikuwa na ustadi wa hali ya juu na usomaji wake wote ulikuwa bora na wa kipekee.

Mmoja wa mabingwa wa Qur'ani alioshawishiwa nao ni mwalimu Mohamed Salamah. Wakati mmoja Ustadh Hassan alipokuwa akisoma Qur'ani kwenye programu katika mji wa Gharbia, Salamah alisikia kisomo chake na akatambua kipaji na umahiri wake. Alimtambulisha Ustadh Hassan kwenye redio ili awe msomaji Qur'ani.

Nukata kuhusu visomo vya wasomaji  Qur'ani katika mkoa Gharbia ni kwamba vingi  vinafanana kabisa. Ingawa qiraa za Mansour Badar na Ali Mahmoud zilikaribiana na za Ustadh Hassan, inaweza kusemwa kwamba Ustadh Hassan alikuwa qari wa kipekee na mtindo wa kipekee.

Mtindo wake ni kwamba inaonekana amechanganya mitindo ya zamani na ya kisasa ya qiraa kisha akaunda mtindo wake mwenyewe. Qiraa yake ina nukta za mtindo ya wasomaji  za zamani na wa kisasa.

Njia ya qiraa inayojulikana kama Tariqa (njia) ya Ustadh Hassan imepewa jina la qari huyu maarufu. Inaonyesha kuwa Hassan ni msomaji mzuri wa Qur'ani Tukufu aliye na ubunifu na tunaweza kusema ameathiri wasomaji wengine zaidi kuliko alivyoathiriwa na wengine.

Baadhi ya visomo vya Ustadh Hassan vinavutia wasikilizaji wa kawaida na vingine vinavutia zaidi wataalamu wa qiraa ya Qur'ani Tukufu. Kwa mfano, usomaji wake wa Surah Hud huvutia wasikilizaji wa kawaida zaidi.

Ustadh Hassan ana baadhi ya visomo 150 vya kazi bora. Nazo ni pamoja na visomo vyake vya Sura Al-Muzzamil, Al-Mutaffifin, Al-Rahman, Al-Muddaththir, An-Naml, Al-Isra, Qaaf, na Adh-Dhariyat.

captcha