IQNA

Ripoti yafichua

Bin Salman kuwaruhusu Waisraeli kununua milki Makka na Madina

12:03 - June 23, 2022
Habari ID: 3475415
TEHRAN (IQNA)- Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad Bin Salman, anatekeleza mpango ambao utawawezesha Waisraeli kununua milki katika miji mitakatifu ya Makka na Madina

Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti 'Saudi Leaks', Mohammad bin Salman maarufu kama MBS, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia ametoa idhini kwa Wazayuni wa Israel kununua milki katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina ili waweze kuimarisha satwa na ushawishi wao.

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na ripoti kuwa Marekani imekuwa ikifanya mazungumzo ya siri ya kupatanisha Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kufanikisha mpango wa kisaliti wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Tel Aviv na Riyadh.

Kwa mujibu wa 'Saudi Leaks' , tayari Saudia inatayarisha mpango wa kuwaruhusu wasiokuwa raia wa nchi hiyo kununua nyumba au ardhi katika miji ya Makka na Madina. Kwa sasa sheria iliyopo hairuhusu raia yeyote asiye Msaudi kumiliki ardhi au nyumba katika miji ya Makka na Madina isipokuwa kwa njia ya urithi tu.

'Saudi Leaks' imeandika kuwa mpango huo wa Saudia wa utapalekea maeneo hayo mawili matakatifu zaidi ya Kiislamu yakumbwa na hatima ambayo Palestina imekumbana nayo baada ya ardhi zao kuporwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israel.

Ripoti hiyo imedokeza kuwa, sasa Bin Salman ameafiki kuwa mashirika ya utawala wa Kizayuni wa Israel na raia wa utawala huo wapewe idhini ya kununua nyumba au ardhi huko Makka na Madina lakini watumie pasi za kusafiria za Marekani na Ulaya.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Utawala wa Kizayuni wa Israel, Yair Lapid alisema kuna jitihada za nyuma ya pazia za kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na Saudi Arabia.

Kwa msingi huo Saudia itajiunga na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco ambazo mwaka 2020 zilitaia saini mapatano ya kuanzisah uhusiano ramsi na utawala haramu wa Israel chini ya upatanishi wa Marekani.

3479423

captcha