IQNA

Uislamu na Ukristo

Msomi wa Kijerumani: Qu'rani Tukufu imesaidia kufafuanua Ukristo

22:24 - May 17, 2022
Habari ID: 3475262
TEHRAN (IQNA) – Msomo wa Kijerumani anaamini kwamba Qur'ani Tukufu imesaidia kuimarisha utambulisho wa Kikristo.

Klaus von Stosch, msomi katika Chuo Kikuu cha Cologne, aliandika katika makala kwamba kisa cha Bibi Maryam (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-SA), mama yake Nabii Issa Masih au Yesu (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS), katika Quran kilisaidia kubatilisha mawazo mengi potofu kuhusu Bibi Maryam (SA).

Alisema kabla ya kuteremshwa Qur'ani Tukufu baadhi ya itikadi za Kikristo zilijaribu kuchafua sura ya mama yake Nabii Issa Masih (AS) lakini fikra zao zilibatilishwa na kuteremshwa kwa aya za Qur'ani Tukufu

Mwanazuoni huyo wa Kijerumani pia alisema kuwa tofauti na baadhi katika Makanisa, Qur'ani Tukufu inauchukulia Ukristo na Uyahudi dini zinazohusiana na kwamba wa Ukristo hajaarifishwa kama dini iliyochukua sehemu ya Uyahudi..

Ameongeza kuwa, Qu'ani Tukufu inalenga kuwaleta pamoja watu wa dini mbalimbali na kusimamisha amani na umoja.

Mzaliwa wa Cologne, Klaus von Stosch amesoma teolojia ya Kikatoliki katika vyuo vikuu vya Bonn na Fribourg.

Mara kwa mara anaandika juu ya mazungumzo ya dini tofauti na mambo ya kawaida kati ya dini za Uislamu, Ukristo na Uyahudi.

4057630

 

captcha