IQNA

Wazayuni watatu waangamizwa katika oparesheni ya Wapalestina ya kujitolea kufa shahidi

18:35 - May 06, 2022
Habari ID: 3475213
TEHRAN (IQNA)-Wazayuni wasiopungua watatu wameangamizwa katika oparesheni za ulipizaji kisasi za Wapalestina waliojitolea kufa shahidi.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni amekiri hasara kubwa iliyopata Israel kutokana na operesheni hiyo ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina katika kitongoji cha El'ad cha mashariki mwa Tel Aviv na kusema kuwa, "tumepata hasara kubwa katika operesheni hiyo".

Vyombo vya habari vya Palestina vilitangaza jana usiku habari ya kuangamizwa na kujeruhiwa Wazayuni kadhaa katika operesheni ya kishujaa iliyofanywa na wanamapambano wa Palestina kwenye kitongoji cha walowezi wa Kizayuni, cha mashariki mwa Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mapema leo Ijumaa, waziri wa usalama wa ndani wa utawala wa Kizayuni, Omer Bar-Lev alikiri kuwa, hadi hivi sasa utawala huo umeshindwa kuwakamata waliotekeleza operesheni hiyo.

Waziri huyo amesema, polisi wa shirika la usalama wa ndani la utawala wa Kizayuni wanaendelea kuwatafuta Wapalestina hao.

Jana usiku walowezi wa Kizayuni walimshambulia waziri huyo wa usalama wa ndani wa Israel wakati alipotembelea eneo la tukio hilo na kumtaka ajiuzulu. 

Kwa upande wake, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Naftali Bennett na baada ya kuitisha kikao maalumu cha masuala ya usalama kuhusu opareseheni ya kitongoji cha El'ad, ametoa vitisho chapwa mapema leo Ijumaa kwa kudai kuwa, waliotekeleza operesheni hiyo watalipa gharama kubwa.

Naye waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni, Benny Gantz ametoa vitisho chapwa kama hivyo akidai kuwa waliofanya operesheni ya El'ad na waliowasaidia, watalipa gharama kubwa.

4054911

captcha